Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585904

Habari Kuu of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kinondoni yaongoza kwa vitendo vya ukatili wa ngono Dar

Kinondoni yaongoza kwa vitendo vya ukatili wa ngono Dar Kinondoni yaongoza kwa vitendo vya ukatili wa ngono Dar

Vitendo vya Udhalilisha na ukatili wa kingono vimetajwa kuongezeka katika Manispaa ya Kinondoni jijini hapa hasa katika kipindi ambacho wanafunzi walikuwa wamefunnga shule kufuatia kuwepo kwa ugonjwa wa Uviko - 19.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 14, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria alisema katika utafiti uliofanywa na LHRC mwaka 2019 hadi 2021 ulibaini vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kingono katika Wilaya ya Kinondoni vimeongezeka na kufikia 57,626.

Vilevile amesema Katika matukio hayo mengi yalikuwa ni yale ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia haswa ule wa kingono yakiathiri zaidi watoto, watu wenye ulemavu, na wanawake kwa mwaka 2020 ambapo janga la Uviko-19 liliingia nchini na kulazimisha shule kufungwa.

“Katika kipindi hicho ambacho watoto walikuwa nyumbani kuliripotiwa kwa matukio hayo haswa yale ya ukatili wa kingono na mimba za utototoni,” amesema.

Amesema kutoka mwaka 2018 hadi 2020 LHRC imekusanya Zaidi ya matukio 2991 ya mimba za utotoni kwa wasichana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 yakiripotiwa katika mikoa mbalimbali, huku kwa mwaka 2020 pekee ikikusanya matukio 448 katika mikoa 15 ya Tanzania Bara.