Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 28Article 566389

Habari Kuu of Thursday, 28 October 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kitabu kitafsiriwe kwa lugha ya kiswahili- Rais Samia

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia ameagiza Chama Cha Wanasheria na Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) na Wadau wa sheria kutafsiri kitabu cha ‘TANZANIA GENDER BENCH BOOK ON WOMEN’S RIGHTS’ kwenda lugha ya Kiswahili.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua kitabu hicho ambacho kinatoa Mwongozo kwa majaji na mahakimu kuhusu haki za wanawake na watoto nchini.

“Naomba nitoe rai kwa TAWJA na wadau wote walioshiriki katika uandaaji wa kitabu hiki kuhakikisha kuwa kinatafsiriwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili ili watu wengi zaidi wakisome lakini pia kukamilika kuandikwa kwa kitabu hichi isiwe mwisho kiwe kinapitiwa muda baada ya muda na kuongeza yale ambayo yanajitokeza jinsi tunavyo kwenda”

“Naomba niwasisitize kutumia lugha yetu ya Kiswahili katika kuandika mienendo ya masharti na hukumu kwani tayari Bunge limeshafanya marekebisho ya sheria kuruhusu matumizi ya kiswahili katika sheria zetu" Rais Samia

Amesisitiza ili serikali iweze kutimiza kikamilifu malengo yaliowekwa kama nchi katika kuwahudumia Watanzania na kuwaletea maendeleo inabidi kutumia lugha inayoeleweka na wengi hususan kwenye mifumo ya utoaji wa haki unaosisitiza usawa kwa watu wote bila kujali hali zao za kijamii na kiuchumi