Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 13Article 557161

Habari Kuu of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kuna Mawaziri walichukulia ukimya wangu kama udhaifu" - Rais Samia

Rais Samia Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kipindi cha miezi 6 ambacho amekua Rais, kuna mengi amejifunza kutoka kwa viongozi mbalimbali ikiwemo Mawaziri ambao walikua wanamsoma na yeye akiwasoma.

Pamoja na hilo wapo baadhi ya Mawaziri ambao Rais amesema kuwa walichukulia hali ya ukimya wake kama udhaifu hivyo kuanza kufanya mambo wanavyojisikia wao.