Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584650

Siasa of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kunambi achukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge

Kunambi achukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge Kunambi achukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge

Mbunge jimbo la Mlimba kupitia CCM, Godwin Emmanuel Kunambi leo January 10, 2021 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni baada kujiuzulu wa Job Ndugai mapema mwezi huu.

Akielezea nia yake hiyo Kunambi amesema kuwa ameamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Spika kwasababu anaamini ana uwezo na sifa zote za kumfanya ashike nafasi hiyo. "Mimi nimekuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na serikali kwa muda mrefu na nimefanya kazi kubwa na nzuri, hivyo naamini ninatosha kuwa Spika wa Bunge na nitafanya kazi kwa weledi na kutenda haki kwa Watanzania na Wabunge wote bila upendeleo" - Godwin Emmanuel Kunambi