Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 26Article 539845

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: millardayo.com

"Kuweni makini mnakopaki magari" Kamanda Wambura

"Kuweni makini mnakopaki magari" Kamanda Wambura

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Camilius Wambura amewataka Wakazi wa Dar es salaam kuchukua tahadhari kwenye maeneo wanayoegesha magari yao sehemu mbalimbali za Jiji kufuatia wimbi la wizi ukiwemo wa magari.

Baada ya Polisi kutoa ripoti ya kukamata Watuhumiwa na magari manne yaliyoibwa Dar huku Watuhumiwa wakitajwa kuiba sana Kinondoni na Ilala, alipotakiwa kutaja mbinu wanazotumia Majambazi hao kuiba magari ili Watu wachukue tahadhari zaidi alisema “Watu wawe makini sana sehemu wanazoegesha magari” Wambura

“Napenda kuwatoa hofu, sisi tumeajiriwa kwa ajili ya usalama wao na mali zao, Watu waishi kwa amani na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi wasiwe na wasiwasi, Polisi imeimarisha doria na misako, doria za miguu na magari kukamata Wahalifu mapema sana kabla hawajatenda uhalifu” Wambura

MTOTO JASIRI ANATANGAZA DW, AWASHANGAZA WENGI, ANA UWEZO WA AJABU, AJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA DUNIANI

Join our Newsletter