Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 08Article 584206

Habari Kuu of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

#LIVE: Full List Mawaziri Wapya na Makatibu Wakuu Hawa Hapa

Rais Samia play videoRais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri huku akiteua mawaziri wapya watano.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Jumanne Januari 4, 2022 Rais Samia wakati akipokea taarifa ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19, Rais Samia alidokeza mpango wa kulifumua baraza lake la Mawaziri.