Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 28Article 554155

Habari Kuu of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Live:Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anazungumza muda huu

Live:Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anazungumza muda huu play videoLive:Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anazungumza muda huu

Ni Agosti 28, 2021 Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa muda huu amekutana na vyombo vya habari anazungumza.

Ayo TV iko live mubashara kutazama kile kinachojiri muda huu.

“Jambo la kwanza ni juu ya maendeleo ya bandari zetu, hali za bandari zetu ni nzuri na zinaendelea kutoa huduma za kusafirisha na kubeba mizigo ndani ya nchi na nje ya nchi kama kawaida licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa inayoikumba dunia janga la  Covid-19“- Msemaji wa Serikali

“Ningependa kuwapa takwimu kidogo katika miezi sita iliyopita Feb-July bandari zetu zilizopo ukanda wa bahari ya Hindi  yaani Tanga, Dar es Salaam na Mtwara na bandari zilizopo katika maziwa yetu yaani Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na zimeongeza idadi ya meli zilihudumia kutoka meli Elfu 1388 ambazo zilihudumia kipindi cha mwaka jana 2020 zimeongezeka hadi kufikia 2206”- Msemaji wa Serikali

“Sasa ongezeko hili kubwa tumelipata  zaidi katika bandari ya Dar es Salaam”– Msemaji Mkuu wa Serikali Gerosn Msigwa