Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 11Article 542263

xxxxxxxxxxx of Friday, 11 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Lowassa amlilia Mzindakaya "alikuwa kiongozi mwenye maono adhimu"

“Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya alikuwa kiongozi mwenye maono adhimu na ya mbali. Aliamini katika uongozi wenye kujali tija na matokeo. Nje ya uongozi alikuwa mfugaji hodari. Alikuwa kada mtiifu wa CCM na msimamizi asiyechoka wa sera za CCM” Waziri Mkuu mstaafu Lowassa 

“Alikuwa msema kweli na mtu mwenye uthubutu. Kwa wale tuliokua nae katika kipindi chake cha ubunge, hatutasahau umakini wake, wa kutumia kanuni kuiamsha serikali pale inapolala. Ni msimamo wake thabiti uliosababisha abatizwe jina la ‘mzee wa mabomu” Waziri Mkuu mstaafu Lowassa 

“Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepo” Waziri Mkuu mstaafu Lowassa 

Ikumbukwe Mzindakaya ndiyo aliongea kutoa wasifu wa Mzee Lowassa wakati alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 2015.

LIVE: BAJETI YA BATA, FAINI ZAPUNGUZWA, BIA PUNGUZO, MADIWANI KULIPWA

Join our Newsletter