Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 584041

Habari za Afya of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

MSD yawafunda Mwananyamala kusafisha damu

MSD yawafunda Mwananyamala kusafisha damu MSD yawafunda Mwananyamala kusafisha damu

Bohari ya Dawa (MSD) imetoa mafunzo ya matumizi ya mashine za kisasa za kusafisha damu kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ili kuwajengea uwezo na umahiri katika kuzitumia mashine hizo.

Machi mwaka jana, Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima alinukuliwa akisema hapa nchini kuna wagonjwa sugu kati ya 4,800 hadi 5,200 wanaohitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikizwa figo, kati ya yao wagonjwa 1,000 wanapata huduma ya usafishaji wa damu kwa sasa.

Hata hivyo gharama za huduma hii zilionekana kuwa ghali na kwa hatua hiyo inayochukuliwa na MSD, katika kufunga mashine hizo inalenga kushusha gharama za huduma hiyo kutoka Sh300,000 ya sasa hadi kufika Sh100,000 kila mgonjwa anapopata huduma kuanzia mwaka huu, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze.

Katika mafunzo hayo ya namna ya kutumia mshine za kutolea huduma hiyo, yalijumuisha watumishi mbalimbali   wakiwemo madaktari, wauuguzi na mhandisi vifaa tiba.

Akizungumza wakati wa kuyafunga mafunzo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Mhidze amesema hatua hiyo inakuja baada ya kuzinunua mashine hizo zinazotarajiwa kusambazwa katika hospitali za mikoa nchini.

Mara baada ya kuwatunuku vyeti, Meja Jenerale Mhidze amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri huko waendako kwa kueneza mazuri waliyojifunza ili hospitali zingine ziweze kuhamasika na kuanzisha huduma hizo za kibingwa katika maeneno yao.

Advertisement “Iwapo kada hiyo ya afya itakubali mabadiliko chanya yanayofanywa na Serikali, kutakuwa na ahueni kubwa kwa wananchi, kwani Serikali kupitia wizara ya afya imedhamiria kupunguza gharama za matibabu, kuboresha miundombinu ya afya.

“Sambamba na kusogeza huduma mbalimbali za afya karibu na wananchi, ikiwamo huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa figo nchini,” amesema Mkurugenzi huyo.

Mratibu wa huduma za magonjwa ya figo nchini, Linda Ezekiel ameishukuru MSD na wadau mbalimbali kwa utayari wao katika kuleta mapinduzi katika matibabu ya kusafisha damu nchini huku akiushukuru uongozi wa Hospitali ya Jeshi Lugalo chini ya Brigedia Jenerali, Dk Fredy Kivamba kwa kukubali kuwa mwenyeji mafunzo hayo.