Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551197

Habari Kuu of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maagizo ya Bashungwa kwa Wakuu Wa Idara nchini kuhusu Corona

Innocent Bashungwa, Waziri wa Saana na Utamaduni Innocent Bashungwa, Waziri wa Saana na Utamaduni

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Wizara yake kupitia Idara za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina wajibu wa kuelimisha umma kikamilifu kuhusu afya na magonjwa mbalimbali ili kuwasaidia wananchi waweze kujikinga na kuchukua tahadhali wakati wote.

Mheshimiwa Bashungwa ameyasema hayo wakati alipozungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo kwenye Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambapo amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia kikamili jukumu hili.

“Naomba kuwaeleza kuwa suala la magonjwa yanayojitokeza kwenye taifa letu ni vita na ili kuvishinda lazima kutumia kila silaha tuliyonayo hivyo, Idara zetu zikitumika vizuri ni silaha kubwa katika kutoa elimu ya afya na magonjwa japokuwa natambua masuala ya afya na magonjwa yanashirikisha pia wenzetu wa Wizara nyingine”

Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili masuala ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo Mhe. Bashungwa ameuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatarishi kwa afya za jamii ambapo amewataka Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakiwa wakuu wa familia zao kuwa makini ili kuzilinda familia zao kwa kuzilinda na hatimaye kuepusha kutoangamiza taifa kwa ujumla.

Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa kuendelea kuhamasisha zoezi la uchanjaji kwa hiari wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 na amewataka wananchi wote kuunga mkono jitihada za Serikali na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwa ugonjwa huo upo na unaua.