Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553627

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maagizo ya Rais Samia kwa polisi kuhusu unyanyasaji mitandaoni

Rais Samia akemea vitendon vya unyanyasaji kupitia mitandao Rais Samia akemea vitendon vya unyanyasaji kupitia mitandao

Mapema hii leo Rais Samia, amefungua kikao kazi cha Jeshi la Polisi, na kulitaka kufatilia kwa ukaribu vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya simu hususiani ya kijamii.

Aidha amelitaka Jeshi hilo kutilia mkazo suala hili kwani linahatarisha si tu usalama wa raia bali taifa kwa ujumla, kwani wengi wa wanaofanya vitendo hivyo wanatumia mitandao ambayo haipo Tanzania.

"Wengi wananyanywasa kwa kupitia mitandao hii, anaemnyanyasa hatumii namba hizi, simu anayotumia inasoma station tofauti tofauti,mara Romani, mara Dubai, na hii ni kwa raia wa kawaida, vipi kwa usalama wa taifa?"-Rais Samia

Ameliagiza Jeshi la Polisi kuja na mkakati utakodhibiti vitendo hivyo kwani vinakwamisha na kutishia amani kwa wanachi wote.