Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573637

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Maagizo ya Silinde Ujenzi wa Madarasa kwa Pesa za Uviko-19

David Silinde David Silinde

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amezitaka halmashauri zote nchini ambazo zinatekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojulikana kwa jina la fedha za ustawi wa maendeleo na mapambano dhidi ya Uviko 19 kujenga kwa kuzingatia ubora na thamani ya halisi ya fedha kuendana na maagizo ya mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa.

Hayo ameyasema akikagua uienzi wa madarasa 26 katika wilaya ya Songwe mkoa wa Songwe kuona utekelezaji wa fedha zilizotolewa na serikali ili kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa nchini kabla ya kuanza kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwakani.

Aidha, Naibu Waziri Silinde amezitaka halmashauri ambazo bado zipo nyuma katika ujenzi wa madarasa hayo kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kufunga taa wakati wa usiku ili kukamilisha ujenzi ifikapo Disemba 15 mwaka huu na kuwapongeza viongozi wa wilaya ya Songwe ambao wamejiongeza kufunga taa baadhi ya shule ili wajenge usiku na mchana waweze kukamilisha kwa wakati.