Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 13Article 557164

Habari Kuu of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maagizo ya Spika Ndugai kwa Waziri Makamba kuhusu mradi wa Stiegler's George

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge, Job dugai, amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, January Makamba kuhakikisha mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler's George unamalizika kwa wakati uliopangwa.

Spika Ndugai ametoa agizo hili wakati wa uapishwaji wa Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika leo septemba 13,2021, Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

“Stiegler’s Gorge lazima imalizike kwa wakati wake, eneo la gesi ni eneo ambalo hapa katikati hatukulipa heshima yake na ni chanzo kikubwa sana cha utajiri, lazima eneo la gesi likafanyiwe kazi vizuri sana lipate heshima yake na nchi ipate mapato ya kutosha zipo nchi zinaendeshwa kwa uchumi wa gesi peke yake,” amesema Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Amesistiza suala hili kwa kutolea mfano wa Jimbo la Kongwa ambalo kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa jimbo hilo lina changamoto ya umeme ambao unakatika karibu mara 30 kwa siku.

“Kuna wakati kule Kongwa umeme unakatika mara 30 kwa siku moja au zaidi, yani ni kitu cha kawaida umeme kukatika sasa lazima tutoke huko na jukumu hili ni la kwako pia January Makamba na hatuwezi Kuwa na maendeleo bila Nishati. Amesisitiza Spika Ndugai