Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552316

Habari za Mikoani of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TAMISEMI

Maagizo ya serikali kuhusu utoaji vibali vya elimu ya msingi

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI,   Gerald Mweli Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerald Mweli

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa anayeshughulikia elimu Gerald Mweli ameagiza utoaji wa vibali kwa miradi mipya inayoanzishwa na wadau wa sekta ya elimu kwa kuangalia utekelezaji wa afua zao katika halmashauri ambazo hazina wadau au zina wadau wachache.

Agizo hilo amelitoa jana wakati wa kufunga warsha ya siku tatu, iliyokutanisha asasa 400 zinazotoa huduma katika elimu msingi nchini yenye kauli mbiu inayosema TUPANGE NA KUTEKELEZA KWA PAMOJA MIRADI YENYE TIJA KWA MAENDELEO YA ELIMU MSINGI

Ameendelea kufafanua kuwa kumekuwa na mtawanyiko usio sawa wa wadau unaochangia ongezeko la tofauti ya ubora wa elimu kimkoa na halmashauri, hivyo amehimiza kuwepo kwa vikao vinavyokutanisha asasi na wadau wa elimu ili kuratibu ushirikiano kati ya Serikali na wadau na kutaka vikao vifanyike katika ngazi ya halmashauri na mikoa.

“ Nawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanaanzidata za wadau wote wanaosaidia katika utoaji huduma katika elimumsingi katika halmashauri zenu na kuandaa vikao vya wadau, angalau vikao vinne kwa ngazi ya halmashauri na viwili katika ngazi ya mikoa kila mwaka kwa lengo la kutathimini utekelezaji miradi kila mwaka” amesisitiza Mweli

Mweli amesema Mikoa ihakikishe inawasilisha taarifa ya utekelezaji wa maelekezo haya kila robo ya mwaka, kwa upande wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutakuwa na vikao mara mbili kila mwaka.

Aidha, ametumia fusra hiyo kutoa rai kwa asasi za kiraia zinashughulika sekta ya elimu kuendelea kuungana na Serikali katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.