Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 09Article 584473

Habari Kuu of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mabadiliko tabia nchi yaanza kuathiri nyumbu Serengeti

Mabadiliko tabia nchi yaanza kuathiri nyumbu Serengeti Mabadiliko tabia nchi yaanza kuathiri nyumbu Serengeti

Mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaendelea sehemu nyingi duniani ikiwamo Tanzania yametajwa kuanza kuathiri mfumo wa nyumbu katika Hifadhi za Taifa ya Serengeti kuzaa kutokana na kuchelewa kwa mvua.

Maelfu ya nyumbu ambao huzunguka Kati ya Hifadhi za Taifa ya Serengeti na Masai Mara nchini Kenya, sasa wamelazimika kubaki eneo la Seronera Serengeti kusubiri mvua ambazo zimechelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Januari 9, 2022, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), William Mwakilema amesema mwaka huu kutakuwa na kuvurugika mfumo mzima wa kuzaa nyumbu.

"Ni kweli, maeneo ya Ndutu udongo una kina kifupi pamoja na kuwa na rutuba, Mvua isiponyesha hakuna malisho. Hawa wanyama instinct kuwa wakienda kule muda huu hakuna malisho ndio maana wanasubiri" amesema

Amesema mvua zikinyesha upande wa Kaskazini wanaweza kuelekea huko lakini mwaka huu kutakuwa na kuvurugika kwa mfumo mzima wa kuzaa, hata ndama watakao zaliwa rate ya kuweza kuishi itakuwa ndogo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete amesema hali kama ya mwaka huu ilitokea pia mwaka 2017.