Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553837

Habari Kuu of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mabalozi wateule nchini wamewasilisha hati za utambulisho kwa Rais Samia

Rais Samia, akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule Rais Samia, akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule

Rais, Samia amepokea Hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wateule wa mataifa mbali mbali yakiwemo ya barani Afrika, mapema hii leo ikulu ya Dar es Salaam

Hatua hii ya upokeaji wa hati hizo, itafungua mianya mingi kwa taifa ikiwemo biashara, lakini pia katika kukuza diplomasia ya taifa kwa ujumla.

Fursa zinginezo zinazopatikana katika mahusiano ya Tanzania na nchi zenye ubalozi hapa nchini, ni pamoja na kukuza sanaaa, michezo, zenye malengo ya kukuza uchumi wa nchi.

Hata hivyo zoezi hilo linatarajiwa kuimarisha mahusiano ya Tanzania na nchi hizo kwa maslahi mapana ya nchi.

Zoezi hilo linaendelea huku mabalozi wakipokezana kuwasilisha hati hizo, na mara baada ya uwasilishaji basi wanakuwa Mabalozi rasmi.

Hati hizo za utambulisho ni kutoka kwa Balozi Mteule wa Nigeria hapa nchini, Hamisu Umar Takalmawa, Balozi Mteule wa India nchini Biyana Srikanta Pradhan na Weibe Jakob De Boer ambaye ni Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini.

Wengine ni Madina Diaby Kassamba Ganou ambaye ni Balozi Mteule wa Burkina Faso hapa nchini mwenye Makazi yake Nairobi, Kenya na Gaussou Touré, Balozi Mteule wa Guinea nchini mwenye Makazi Addis Ababa, Ethiopia.