Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559948

Habari za Mikoani of Monday, 27 September 2021

Chanzo: Wasafifm

Mabasi 10 yazuiwa kusafirisha abiria Tabora

Mabasi Mabasi

Jeshi la polisi Mkoa wa Tabora limeendesha msako maalumu wa kuondosha magari yote mabovu ya kubeba abiria ndani ya stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora .

Katika msako endelevu ambao umefanyika September 27 kuanzia majira ya saa kumi na moja alfajiri ukiongozwa na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Tabora SP. Gabriel Chiguma amesema mbali na kuondosha Magari yote mabovu yanayobeba abiria kwenda mikoani pia msako huo ndani yake umelenga kupunguza wimbi la ajali ambazo zimekuwa zikitokana na ubovu wa magari.

Aidha katika msako huo jumla ya magari 10 ya abiria yamezuiliwa kuendelea na safari zake mpaka yatakapo kamilisha matengenezo yaliyoelekezwa na Jeshi la Polisi ikiwemo ubovu wa mabodi, matairi, breki pamoja na mivujo ya mafuta katika sehemu za Injini.

Hata hivyo, abiria wamesema zoezi la magari kukaguliliwa ni muhimu kuwa endelevu kutokana na gari nyingi zimekuwa zikitumika na wamiliki barabarani hali kuwa ni mbovu.