Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 15Article 542836

Habari Kuu of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mabehewa treni ya kisasa kuhifadhi nishati kwa saa mbili-Waziri

Mabehewa treni ya kisasa kuhifadhi nishati kwa saa mbili-Waziri Mabehewa treni ya kisasa kuhifadhi nishati kwa saa mbili-Waziri

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mabehewa ya treni ya umeme itakayokuwa ikifanya safari kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme kwa muda wa saa moja hadi mbili bila kuzima.

Amesema hayo leo wakati wa Mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na Vijana uliofanyika Nyamagana, mkoani Mwanza huku akieleza maendelo ya mradi huo wa reli ya kisasa.

Dk Kalemani amesema kuwa, hadi sasa ujenzi wa kipande cha reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro umeshakamilika.

Aidha, amewasihi vijana kutumia fursa zitakazotokea kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kutumia treni hiyo kwa kusafirishia bidhaa zao kwenda sehemu mbalimbali .