Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 26Article 539947

Habari Kuu of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mabeyo apongezwa kuendeleza michezo

Mabeyo apongezwa kuendeleza michezo Mabeyo apongezwa kuendeleza michezo

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amepongezwa kwa jitihada zake za kuendeleza michezo baada ya kujenga uwanja wa gofu jijini Dodoma.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Waitara wakati akizindua kivuko na kibanda cha kupumzikia wachezaji wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Lugalo, Dar es Salaam jana.

“Mwanzo tulipata eneo yatakapojengwa Makao Makuu ya Jeshi Dodoma lakini ilikuwa mbali ila kwa Kilimani ni eneo sahihi,” alisema.

Jenerali Waitara alisema uwanja huo utamfanya mkuu huyo wa majeshi kuacha kumbukumbu za heshima.

“Jeshi ni mfano na linaongoza katika kuhamasisha michezo yote nchini na halijawahi kushindwa, hivyo ni mwendelezo mzuri,” alisema Jenerali Waitara.

Alisema ujenzi wa uwanja wa gofu sio mgumu na kinachotakiwa kufanyika ni kuchukua kilichofanyika klabu ya gofu ya Lugalo

kuhamishia Dodoma.

Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo alipongeza wanachama wanaojitoa kutatua changamoto za uwanja huo.

Aidha, alitoa wito kwa wachezaji wenye nia njema kujitokeza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uwanja huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Timu ya Majenerali na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa aliwahamasisha viongozi wa serikali kucheza mchezo huo.

Alisema gofu ndio mchezo pekee unaoweza kuchezwa kwa muda mrefu bila kujali umri na idadi ya wachezaji.

Ujenzi wa kidaraja umefanikishwa kwa hisani ya Profesa Wineaster na kibanda cha kupumzikia kimejengwa na Mike Laizer.

Join our Newsletter