Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 25Article 559630

Habari za Mikoani of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Machinga Iringa wagoa kuondoa sehemu zilizokatazwa

Machinga Iringa wagoa kuondoa sehemu zilizokatazwa Machinga Iringa wagoa kuondoa sehemu zilizokatazwa

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo (machinga) wa Manispaa ya Iringa wamesema kuwa hawapo tayari kuondoka katika eneo la Mashine Tatu na Miomboni kwa kuwa maeneo hayo ndio ambayo yanawateja wengi wanaonunua bidhaa kwa wingi tofauti na maeneo mengine ya manispaa.

Wakizungumza kwenye mkutano waliofanya na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu walisema kuwa wanaheshimu na kufuata maagizo yote ya Waziri Mkuu, Aidha, machinga  hao walisema kuwa wanaiomba serikali ya manispaa ya Iringa kufuata maagizo ya Waziri mkuu ambayo aliyatoa kuhusu namna ya mpangilio mzuri wa wafanyabiashara wadogo wadogo.

Walisema kuwa wamekuwa wanachangia mapato serikalini bila tatizo  na kukuza uchumi wa Manispaa  kwa ujumla iwaje ghafla wanataka kuwaondoa kwenye maeneo ambavyo wamezoea kuyafanyia kazi kila siku.

Kwa upande wake katibu wa Machinga Network mkoa wa Iringa, Joseph Kilienyi alisema kuwa serikali ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa alisema kuwa wafanyabiashara hao wapo tayari kupangwa kwenye maeneo wanayofanyia baishara na sio kuondolewa kwenye maeneo hayo ambayo wamekuwa wanafanyia baishara kwa miaka mingi bila kusumbuliwa.

Alisema kuwa kuwaondoa machinga kwenye maeneo ambayo wanayafanyia kazi litakuwa jambo gum una haliwezekani hata siku moja hiyo ni lazima serikali ijipange kuhakikisha inatatua jambo hilo kwa kufuata muungozo wa Waziri mkuu.

Kilienyi alisema kuwa anaamini kwenye majadiliano tofauti na kutumia nguvu kama ambavyo baadhi ya viongozi kwenye maeneo mengine wamekuwa wakitumia nguvu kuwaondoa machinga kwenye maeneo ambayo wameyazoea kufanyia  biashara zao.

Alisema kuwa wapo tayari kufuata sheria zote za nchi na kuondoka katika maeneo hatarishi kama kwenye mifereji na maeneo mengine kama hayo lakini sio maeneo ambayo wanataka kuwapeleka hivi sasa ambayo kwa kiasi kikubwa sio rafiki na biashara zao.

Kilienyi alisema kuwa wafanyabiasahara wadogo wadogo wamekuwa wanafanya biashara zao katika maeneo hayo kama mbadala wa kuajiliwa na serikali kwa kuwa hivi sasa ajira zimekuwa ngumu kupatika hivyo njia mbadala ni kufanya biashara.Alisema kuwa kuwaondoa machinga katika maeneo ambayo wamezoea kuyafanyaia kazi ni kupunguza kasi ya kukuza uchumi wananchi na kufifisha maendeleo ya nchi kwa kuwa machinga wamekuwa msaada mkubwa kwa serikali kukuza uchumi wa nchi na kuongeza thamani ya mitaji ya matajiri.

Kilienyi alisema kuwa hawapo tayari kuondolewa katika barabara ya mashine tatu bali wapo tayari kupangwa kwenye mpangilio mzuri unaostahili hivyo uongozi wa halamshauri ya Manispaa ya Iringa wanapaswa kufikiri upya kuhusiana na mpango wao.

Naye mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu aliwataka wafanyabiashara waodogo wadogo kuwa na subira wakati serikali ya halmashauri ya Iringa wakijipanga kuhakikisha wanatatua mgogoro huo na kuwapanga vizuri kwenye eneo hilo la mashine tatu ambalo limekuwa na mzunguko mkubwa wa biashara.Alisema kuwa machinga wanatakiwa kupangwa kwenye mpangilio mzuri ambao utakuwa rafiki kwao wakati wa kufanya biashara zao. Msambatavangu aliwataka wamachinga kuwa wasafiri na kuondoka mara moja kwenye maeneo hatari ambayo yamekuwa yanaathiri afya zao na mienendo ya biashara zao kwa ujumla.

Alimalizia kwa kusema kuwa serikali ya halmashauri ya wilaya ya Iringa wapo kwenye mjadala wa namna gani wafanyabiashara hao watafanya baishara zao bila kusumbuliwa na mtu yeyote yule.