Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 12Article 585226

Habari Kuu of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Maeneo ya Dar, Kibaha Kukosa Maji kwa Saa 16

Maeneo ya Dar, Kibaha Kukosa Maji kwa Saa 16 Maeneo ya Dar, Kibaha Kukosa Maji kwa Saa 16

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 16 kuanzia saa 12 jioni tarehe 12/1/2022 hadi 13/1/2022.

Sababu: Kuruhusu matengenezo ya miundombinu ya bomba la inchi 36 Mtamboni na inchi 48 eneo la Visiga seminary.

Maeneo yatakayoathirika ni;

Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Disunyura, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi magari saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara, Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara b, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, na Ubungo.