Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540478

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Magige na genge lake waichefua CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani ukiukaji maadili unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige

Magige akiwa na baadhi ya wanawake, walivamia msiba wa marehemu Kudula Madoda hali iliyosababisha sintofahamu wakati maziko yakiendelea.

Taarifa ya CCM kutoka Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ilisema CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

“Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM,” alisema.

Join our Newsletter