Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554638

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mahakama Kutoa Maamuzi kesi ya Mbowe sept 1, 2021

Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kesho Jumatano Septemba 1, 2021 itaamua pingamizi la Mbowe na wenzake kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi yao ama la.

Mbowe na wenzake wameipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Jaji Elinazer Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano asubuhi atakapotoa uamuzi.