Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559357

Habari Kuu of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi ya Mbowe

Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi ya Mbowe Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi ya Mbowe

Mahakama Kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kupinga utaratibu uliotumika katika kumkamata, kumuweka kizuizini na kumfungulia kesi ya ugaidi.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji John Mgetta, baada ya kukubaliana na hoja ya Serikali kwamba ombi la Mbowe halikuwa sawa na linakinzana na kifungu cha 4(5) na kifungu 8(2) cha Sheria ya msingi na utekelezaji wa majukumu Sura namba tatu.

Jaji Mgetta amemweleza mlalamikaji kupeleka lalamiko lake katika Mahakama ya Uhujumu Uchumi.