Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541480

Siasa of Monday, 7 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Mahakama haina jengo Bunge imepanga" Bulaya

"Mahakama haina jengo Bunge imepanga" Bulaya

Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, amesema kuwa wilaya ya Bunda haina jengo la Mahakama badala yake wafanyakazi wa Mahakama wamebakia kuendesha shughuli zao kwenye nyumba za kupanga.

Bulaya ametoa kauli hiyo bungeni Jijini Dodoma, wakati akiuliza swali kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu ni lini sasa serikali itahakikisha Mahakama ya wilaya hiyo inakuwa na jengo lake kabisa.

“Wilaya ya Bunda haina jengo la Mahakama imepanga kwenye nyumba ya Mzee Wasira kwa muda mrefu, sasa hivi wameamua kupanga kwenye nyumba nyingine, je ni lini wilaya hiyo itakuwa na jengo la Mahakama?” Bulaya.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda amesema “Kufikia 2025 sehemu zote ambazo hazina Mahakama za wilaya na makao makuu ya Tarafa zote katika ngazi ya Kata zitakuwa na majengo mapya, tuvumilie tutaendelea kuazima majengo ila 2025 ni mwisho”.

WOSIA WA TB JOSHUA KUELEKEA BIRTHDAY YAKE “HAITAKUWA RAHISI, SITOWEZA KUSHEREHEKEA”

Join our Newsletter