Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560311

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mahakama ya Haki Afrika kuboresha mfumo wa usikizaji wa kesi

Mahakama ya Afrika kuboresha mfumo wa usikizaji wa kesi Mahakama ya Afrika kuboresha mfumo wa usikizaji wa kesi

Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika, Jaji Iman Abood, amesema mahakama imetengeneza mifumo mbalimbali ya kusikiliza kesi katika kipindi cha Rais mstaafu wa mahakama hiyo Jaji Sylvain Oré, ikiwa ni mipango ya kuiongezea ufanisi Mahakama hiyo katika utendaji wake wa kila siku.

Jaji Abood, ameyasema hayo jijini Arusha katika hafla ya kumuaga Rais Sylvain Oré, aliyemaliza muda wake wa kuiongoza mahakama hiyo huku akitajwa kuweka mifumo pamoja na idadi ya wafanyakazi iliyo wezesha mahakama hiyo kufanya kazi kwa ustadi mkubwa.

"Mahakama imeweza kutengeza mifumo ya usikilizaji na uhifadhi wa kesi , pamoja na kuongeza watumishi wakutosha wa Mahakama ili kurahisha usikilizaji wa mashautri yanayofika katika Mahakama hii" Jaji Abood.

Aidha ameongeza kusema kuwa Mahakama hiyo itaendelea kutimiza majukumu yake kwa weledi, ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa usawa, pamoja na kuharakisha usikilizwaji wa mashauri yanayofikishwa Mahakamani hapo