Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541732

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mahakama yaihoji Jamhuri kuchelewa kesi ya Lissu

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema hayo jana wakati kesi hiyo ikitajwa na upande wa Jamhuri kudai mshtakiwa Lissu bado yuko Ujerumani.

"Kesi imesimama muda mrefu, nimefumbia macho siku nyingi sana, Wakili wa Jamhuri hebu tuelezee,"alisema Hakimu Simba.

Akijibu Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanton, alidai shauri lilisimama sababu ya Lissu hayupo nchini.

Hakimu Simba alihoji kwamba kesi ya muda mrefu na vifungu vya sheria kadhaa vipo vinavyozungumzia mazingira kama hayo ambapo mshtakiwa anakuwa hayupo kwa muda mrefu.

Wakili Mitanto alidai kuna maombi ya wadhamini wa Lissu ya kujitoa kwenye udhamini endapo yatatolewa uamuzi yatatoa muongozo kwa upande wa kesi ya jinai.

Hakimu Simba alikubali hoja hizo na kuamuru kwamba pingamizi la Jamhuri lililowasilishwa kwenye maombi ya wadhamini litasikilizwa kisha uamuzi utatolewa ili kupata muongozo wa kesi ya jinai inayokwama kuendelea.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Julai 7 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza pingamizi la Jamhuri kwenye maombi na kuitaja kesi ya jinai.

Wadhamini wa Lissu waliomba kujiondoa kumdhamini mshtakiwa huyo na kuiomba mahakama iyatupilie mbali.

Miongoni mwa hoja katika pingamizi la upande wa Jamhuri ni kwamba Mahakama haiwezi kushughulikia jambo hilo na haina Mamlaka ya kusikiliza na kutolea uamuzi maombi hayo hivyo wanaomba yatupwe.

Katika kiapo kinzani Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo anadai Lissu aliruka dhamana tangu tarehe aliyopona na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Join our Newsletter