Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553117

Uhalifu & Adhabu of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mahakama yatupilia mbali pingamizi la sabaya

Mahakama yatupilia mbali pingamizi la sabaya Mahakama yatupilia mbali pingamizi la sabaya

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya unyang'anyi wakutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Mawakili upande wa utetezi waliweka pingamizi dhidi ya Mawakili wa Jamhuri kumhoji mshitakiwa namba mbili, Sylvester Nyengu kuhusu nyaraka ambayo mshatikwa alisema Agosti 20 haitambui wakati wa utetezi.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo anayesikiliza kesi hiyo yenye mvuto mkubwa amesema Mawakili wa upande wa Jamhuri wanaweza kuendelea kumhoji mshtakiwa.

"Katika sehemu ya hoja ya maswali ya dodoso (cross examination) haina kikomo, shahidi au mshitakiwa anaweza kuulizwa maswali yoyote kuhusu kielelezo hatakama hakitambui," ameamua Amworo.

Baada ya maamuzi hayo yaliyotolewa mapema leo Agosti 23, Mahakama inaendelea kusikiliza na kuhoji utetezi wa Mshitakiwa namba mbili Sylvester Nyengu.