Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 09Article 550471

Habari Kuu of Monday, 9 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Mahakamani:Mbowe awashtaki Viongozi wa ngazi ya juu akiwemo IGP (Video+)

Mahakamani:Mbowe awashtaki Viongozi wa ngazi ya juu akiwemo IGP (Video+) play videoMahakamani:Mbowe awashtaki Viongozi wa ngazi ya juu akiwemo IGP (Video+)

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kumruhusu Mbowe kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya ambapo litatajwa Agosti 30, 2021. Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kakosa la ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kuhusiana na mashtaka hayo, huku akieleza maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi.