Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 09Article 584437

Uhalifu & Adhabu of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Maiti ya mtoto yafukuliwa Handeni, yatupwa mtaani

Maiti ya mtoto yafukuliwa Handeni, yatupwa mtaani Maiti ya mtoto yafukuliwa Handeni, yatupwa mtaani

iku moja baada ya mwili wa mtoto Sharifa Abasi kuzikwa, kaburi lake limefukuliwa na watu wasiojulikana huku mwili wake ukikutwa umetupwa mtaani ukiwa bado ndani ya sanda.

Mwili wa mtoto ambaye aliyefariki akiwa na mwezi mmoja na wiki mbili ulizikwa jana Jumamosi Januari 8, 2022 umekutwa katika mtaa wa Msasa Shule wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akisimulia mkasa huo baba mkubwa wa marehemu, Athumani Ligotwe wakati wa mazishi ya pili ya mtoto huyo yaliofanyika leo Jumapili asubuhi amesema ameshangazwa na tukio hilo kwani yeye ndio aliweka mwili wa marehemu kaburini jana na leo wamekutwa kaburi limefukuliwa na mwili haupo.

Amesema alifika kwenye kaburi na kubaini mwili haupo na kurudi sehemu ambayo umeonekana na kuthibitisha kuwa ulikuwa wa mtoto wa mdogo wake ambaye alizikwa jana.

"Hili ni tukio la kinyama sana lililotokea kwenye familia yetu, wamefukua kaburi ya mtoto wetu na kwenda kutupa mwili mita 300 kutoka hapa kwenye nyumba ya mtu, tunaomba Jeshi la Polisi kuwatafuta hawa watu", amesema Athumani

Mkazi wa Msasa, Deo Akyoo ambaye mwili wa mtoto umekutwa kwenye uzio wa nyumbani kwake amesema usiku alisikia watu wakipita na baada ya kuamka asubuhi aliangalia na kukuta mwili wa mtoto huyo upo kwenye sanda akatoa taarifa katika uongozi wa mtaa.