Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573943

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Majaliwa Atoa Maagizo kwa Wizara Hizi

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza wizara zote zenye dhamana ya ukuzaji ajira kuhakikisha zinaandaa programu na mikakati bora ya ukuzaji ajira ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wote nchini washiriki katika utekelezaji wake ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira.

Pia, Majaliwa amezielekeza Ofisi na Wizara zote zenye dhamana za uwekezaji na biashara zihakikishe zinashirikiana na wadau wengine hususan sekta binafsi kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kutoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vitakazochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.

Ametoa maagizo hayo jana (Jumatano, Novemba 24, 2021) wakati akizindua Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Soko la Ajira kutokana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020/2021. Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar.

Majaliwa amesema kuwa idadi ya watu walio na ajira nchini imeongezeka kutoka watu milioni 20.5 mwaka 2014 hadi kufikia watu milioni 24.1 mwaka 2020/2021, sawa na ongezeko la asilimia 17.5, ambapo kati yao wanaume ni milioni 12.4 na wanawake ni milioni 11.7.