Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551326

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Majaliwa Awataka Ma-RC Kutolaza Fedha za Miradi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amezungumza na Wakuu wa Mikoa kwa njia ya mtandao (Video Conference) ambapo amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi tangu ameingia madarakani na hivyo kuwataka Wakuu wa Mikoa kuzisimamia fedha zinazotumwa kutoka TAMISEMI na Mamlaka ya Elimu nchini (TEA) ili kuhakikisha kuwa zinafanya kazi katika muda uliopangwa.

“Fedha ikija haipaswi kukaa zaidi ya wiki, ni lazima ziende kwenye maeneo ya utekelezaji"

Amewataka pia Wakuu wa Mikoa waendelee kusimamia mazao ya kimkakati kama alizeti, chikichi, parachichi na sasa tunaimarisha mazao ya ufuta, kokoa, Zabibu katika maeneo yao.

Kuhusu ulinzi na usalama, Waziri Mkuu amesema viongozi wanapaswa kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa kutosha nchini ili watu waweze kufanya kazi kwa amani.

“Pakiwepo usalama baina koo na koo, kijiji na kijiji, itasaidia kufanya kazi na kuongeza uzalishaji”