Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572362

Habari Kuu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Majaliwa asisitiza riba za mikopo ya benki kushuka

Majaliwa asisitiza riba benki kushuka Majaliwa asisitiza riba benki kushuka

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kukaa na benki na kuangalia namna ya kuweka masharti na riba nafuu ya mikopo kwa taasisi au kampuni zinazotaka kuanzisha viwanda nchini.

Akizindua jengo la kiwanda cha kutengeneza kemikali za ujenzi cha Sika kilichojengwa Mbezi-Salasala jijini Dar es Salaam, alisema inaendelea na mpango wa kutaka kuona Tanzania inakuwa ya viwanda kwa ajili ya ustawi wa uchumi na kwamba ni lazima waweke mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwapo kwa masharti na riba nafuu kutavutia taasisi na kampuni kukopa kwa ajili ya uwanzishwaji wa viwanda, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

"Mbali na maagizo haya kwa Wizara ya Fedha, lakini pia zipo jitihada zinazofanywa na wawekezaji kwa kujenga viwanda nchini na kushiriki kwa vitendo maono ya serikali ya kutaka kuwa na viwanda vingi,”alisema.