Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541783

Habari Kuu of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Majaliwa ataka mwarobaini kuzorota michezo Tanzania

Majaliwa ataka mwarobaini kuzorota michezo Tanzania Majaliwa ataka mwarobaini kuzorota michezo Tanzania

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania bado haijafanya jitihada za kutosha katika kuwaandaa wanamichezo wake kushiriki medani za kimataifa.

Amesema sababu hiyo ni kuotokana na wizara pamoja na wadau wanaohusika na michezo nchini kutoimarisha msingi wa michezo kuanzia ngazi ya shule za awali.

Kufuatia hatua hiyo, Majaliwa ameziangiza wizara na mamlaka zote zinazosimamia meandeleo ya Sanaa na michezo nchini kuwajibika kikamilifu na kutafuta mbinu za kuboresha michezo nchini.

Majaliwa ametoa kauli wakati akizindua Mashindano ya kitaifa ya michezo na Taaluma kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA), ambayo yanfanyika mkoani hapa.

Amesema yapo malalamiko mengi kuhusu wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri ndani na nje ya nchi, hivyo viongozi na wadau wengine wa michezo wanapaswa kukaa chini na kujiuliza sababu na kisha kufanya jitihada za kukuza na kuendeleza vipaji ili waweze kuchangia kwenye uimara wa michezo nchini.

Ameeleza kuwa taifa likijiimarisha na kuwekeza katika michezo itasaidia kujenga misingi imara kwa wanamichezo, ambao utasaidia kuwapa manufaa ya kuajiriwa, kujenga moyo wa kujiamini, mshikimano na kujenga afya.

Aidha Majaliwa ameagiza kufanyiwa tathimini kwa mitaala ya elimu nchini ili iweze kujielekeza katika kujenga stadi za ujuzi kwa maendeleo ya kizazi kimoja hadi kingine kwenye michezo, kwa kuboresha mazingira ya vyuo vilivyokuwa vinatoa elimu ya michezo, kuongeza ajira za walimu wa michezo, kuandaliwa mashindano na kalenda za michezo ili iweze kuleta tija kwa taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, utamaduni sanaa na michezo Innocent Bashungwa amesema, Wizara hiyo inatarajia kuanzisha kituo maalumu cha kuendeleza michezo (centre of sports excellence) katika chuo cha maendeleo ya michezo Mkoani Mwanza, Ili kuendeleza vipaji vinavyovumbuliwa katika mashindano hayo ya kitaifa ya michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari.

Amesem wizara yake kwa kushirikian na ofisi ya Rais Tamisemi na wizara ya elimu, serikali inaendelea kufanya tathimini katika kila mkoa ili kubaini shule maalumu zitakazopendekezwa kwa ajili ya kuendeleza vipaji.

Mashindano haya ya Kitaifa ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari yanajumuisha wanafunzi kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara na Visiwani, ambapo wanafunzi wanashindana katika michezo mbalimbali ya Mpira wa Miguu, mpira wa pete, mpira wa goli, mpira wa wavu, riadha jumuishi, kwaya na ngoma na kadhalika.

Join our Newsletter