Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572569

Habari Kuu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Majaliwa awataka Watanzania kuwekeza kwenye vyakula rutubishi

Majaliwa awakata Watanzania kuwekeza kwenye vyakula rutubishi Majaliwa awakata Watanzania kuwekeza kwenye vyakula rutubishi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwekeza kwenye sekta ya uchakataji na usindikaji wa vyakula vyenye virutubishi ili kupunguza idadi ya watu wenye utapiamlo.

Kauli hiyo inakuja kufuatia baadhi ya mikoa nchini ambayo inazalisha chakula kwa wingi kuwa na ongezeko la watoto wenye lishe duni ikiwamo Njombe, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Songwe na Kigoma huku mkoa wa Tanga ukiwa ni mkoa ambao awali ulikuwa chini kwa asilimia 23 kwa mwaka 2014 lakini kwa miaka ya hivi karibuni mkoa huo umekuwa na takwimu zinazoongezeka hadi kufikia asilimia 34.

Waziri aliyasema hayo wakati wa mkutano wa saba wa wadau wa lishe uliofanyika mjini Tanga, sambamba na uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Masuala ya Lishe wa miaka mitano awamu ya Pili (NMNAP) huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta ya chakula na lishe kuwekeza kwenye utafiti na uzalishaji wa bidhaa za vyakula vyenye virutubishi.

''Sisi kama Serikali tupo tayari kuwawezesha wawekezaji kuanzia viwanda vidogo hadi vikubwa lakini pia kwa sasa hivi wapo wazalishaji wa mtu mmoja mmoja hususani wanaotengeneza unga na chumvi majumbani , wote hao ni watu muhimu kwetu" alisema Kasimu Majaliwa

Aidha aliwataka wadau wa lishe nchini kuanzia ngazi ya mtaa , halmashauri na Taifa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya serikali ili kuleta mafanikio ,

kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Lishe Bora ni msingi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Uchumi Shindani.

"Napenda niwaambie wadau wetu wa lishe kuwa tutekeleze kwa vitendo kaulimbiu yetu ili tupate matokeo chanya kwenye taifa letu, tuweke virutubishi kwenye usindikaji wa vyakula"

Alisema Serikali imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji wa usindikaji wa bidhaa lishe hapa nchini,

"Rasilimali watu ndio msingi mzuri wa kutokomeza umaskini nchini kwetu lakini pia lishe bora ndio msingi wa afya za watu na husaidia kuipunguzia serikali mzigo wa gharama za kimatibabu kwa wananchi wake "alisisitiza Majaliwa

Kwaupande wake Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Vijana , Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Muhagama alitaja baadhi ya mikoa nchini kwa kiwango chake inavyoendelea kuongoza kwenye udumavu kutokana na lishe duni kuwa ni Njombe 53.6%, Rukwa 47.9%, Iringa 47.1%, Songwe 43.3% kigoma 42.3% na Ruvuma 41.1% .

Alisema elimu juu ya lishe inapaswa kutolewa kwa wananchi ili watumie vyakula wanavyolima wenyewe kwa lengo la kuondokana na utapiamlo ikiwamo udumavu.