Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 20Article 558574

Habari za Mikoani of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Majanga ya asili yakimbiza watu 100,000

Mafuriko Mafuriko

Majanga ya Asili yamesababisha Watu kukimbia makazi yao miaka ya karibuni, ikielezwa wengi wao walikuwa wakiishi pembezoni mwa Ziwa Tanganyika ambapo viwango vya maji vimeongezeka na kusababisha mafuriko na maporomoko

Shirika la Save The Children linasema takriban 85% ya Watu 122,500 wanaokaa kambini Burundi wamehama makazi yao kutokana na majanga hayo na sio vita.

Watoto wametajwa kuathiriwa kwa kiasi kikubwa ikielezwa Watoto wapatao 7,200 chini ya mwaka mmoja wanaishi kwenye Kambi zinazohudumia waliokubwa na majanga.

katika kambi ya Gatumba yenye wahanga wa mafuriko 3000 zaidi ya asilima 80% ni watoto. Wengi wao hawasomi na pia wanaishi kwa kupata mlo mmoja kwa siku.

Mama mmoja mwenye watoto watatu, 47, amesema hofu yake kubwa ni wanae wanaweza kufa kwa njaa.

" nilikuwa mkulima lakini sasa nyumba yangu imekwenda na maji"