Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 08Article 541603

Habari Kuu of Tuesday, 8 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Maji kukosekana June 8 hadi 9, DAWASA waomba radhi

Maji kukosekana June 8 hadi 9, DAWASA waomba radhi Maji kukosekana June 8 hadi 9, DAWASA waomba radhi

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa saa 24 kuanzia tarehe 8/6/2021 asubuhi hadi 9/6/2021.

Sababu ya kukosekana kwa maji ni matengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji 54 linalotokea katika matenki ya chuo kikuu Ardhi eneo la Victoria na Makumbusho baada ya kupasuka.

Maeneo yatakayoathirika ni Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa ndege, Tegeta, kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach, Mlalakuwa,Mwenge, Mikocheni, Msasani, sinza, kijitonyama, oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji (City center), Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, hospitali ya Rufaa Mhimbili, Kigamboni Navy na Ferry

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

WEZO WA MTOTO WA UWOYA KUCHEZA MPIRA “BABA NA RONALDO WANANIVUTIA UWANJANI”

Join our Newsletter