Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573730

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: eatv

Maji kurejea maeneo haya Dar es Salaam

Maji kurejea maeneo haya Dar es Salaam Maji kurejea maeneo haya Dar es Salaam

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa leo amefungua mtambo wa kuruhusu maji kwenda maeneo ya Survey, Masaki, Mikocheni, Kawe, Tegeta, Mbweni, Makumbusho, Kijitonyama, Mwananyamala na Mjini Kati, na kuwasihi wananchi kuhifadhi maji na kuwa wamoja kuliko kipindi chochote kile.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Waziri Aweso, amewaomba wananchi kutunza maji huku wizara hiyo akiahidi kwa kushirikiana na DAWASA kuwa imara na kupambana kwa uwezo wao na kuwaomba viongozi wa dini kuiombea nchi kupata mvua za baraka.

"Niwaombe sana kipindi hiki tuhifadhi maji kwa wingi na zaidi niwasihi sana tuwe wamoja kuliko kipindi chochote kile, watumishi wa DAWASA na Wizara ya Maji tuwe imara tupambane kwa uwezo wetu wote, viongozi wa dini kesho siku ya ibada tuiombee nchi yetu kupata baraka ya mvua na naamini tutavuka salama kipindi hiki kigumu," ameandika Waziri Aweso.