Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540685

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Makala aombwa kuondoa mgogoro Tarura, Jiji la Dar

NAIBU Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji, amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutatua mgogoro uliopo kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutowachanganya wananchi kuhusu ukusanyaji wa mapato ya magari yanayoegeshwa pembezoni mwa barabara kinyume cha sheria.

Akizungumza katika Kikao cha Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, Khimji alisema mgogoro huo umekuwa ukiwachanganya wananchi.

Alisema kumekuwa na hali ya gari kukamatwa na Tarura kwa kosa la kuegesha katika eneo lisiloruhusiwa, lakini dakika chache baadaye, mhusika huyohuyo anakamatwa tena na askari wa Jiji la Dar es Salaam kwa kosa hilohilo.

Aliomba Mkuu wa Mkoa, Makala, kutoa maelekezo kati ya Jiji la Dar es Salaam na Tarura juu ya ukusanyaji wa kodi hiyo.

Join our Newsletter