Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 15Article 586075

Habari za Mikoani of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Makamu wa Rais asimamisha mkataba wa usafi jijini Dodoma

Makamu wa Rais asimamisha mkataba wa usafi jijini Dodoma Makamu wa Rais asimamisha mkataba wa usafi jijini Dodoma

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameagiza kusimamishwa kwa mkataba kati ya Jiji la Dodoma na Kampuni ya ‘Green Waste’ inayokusanya takataka kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kiufanisi.

Akizungumza na viongozi wa jiji hilo leo Januari 15, 2022 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maeneo, Dk Mpango amefikia uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na hali ya usafi katika jiji hilo.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais ametembelea Soko la Majengo na kushudia uwepo wa takataka katika maeneo mbalimbali ambazo wananchi wamezikusanya na huchukua muda mrefu pasipo kuondolewa.

Amewataka viongozi wa Jiji la Dodoma kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi pamoja na maeneo ya masoko na barabara zote.

Aidha, Makamu wa Rais amewaagiza wakurugenzi katika maeneo mengine nchi nzima kuchukua zoezi la usafi kama zoezi endelevu na linapaswa kuzingatiwa kikamilifu.

Amewataka viongozi kuacha kukaa ofisini pekee bali pia kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo yao ili kufuatilia wale waliowapa dhamana ya uondoaji wa takataka hizo katika mitaa kama wanakidhi kuendelea kufanya kazi hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amemuhakikisha Makamu wa Rais kwamba ndani ya wiki mbili jiji la Dodoma litakua safi na hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kuwataka viongozi wa Wilaya kuanzia leo tarehe 15 Januari kuzungumza na wafanyabiashara pamoja na kupata muafaka wa namna bora ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira katika maeneo