Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552754

Habari za Mikoani of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Makato ya Tozo Kujenga daraja la juu jangwani

Makato ya Tozo Kujenga daraja la juu  jangwani Makato ya Tozo Kujenga daraja la juu jangwani

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema tozo mbalimbali zinazokatwa zinaenda kufanya shuguli za maendeleo na kwamba serikali ina mpango wa kujenga daraja kubwa maeneo ya Jangwani ambako panakumbwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati zam mvua.

Mwigulu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam na kudai kuwa nchi ina miradi ya kimkakati ni lazima iendelee na moja ya miradi ni kujenga daraja la juu la kisasa Jangwani.

“Haya matatizo mmeshahangaika sana mara mnavua samaki Jangwani, mnakimbia Jangwani mpaka klabu yangu ninayoipenda inataniwa, Rais Samia atapiga daraja moja Magomeni hadi Fire juu kwa juu yaani ukiwa kule unakuwa kama unataka kuwa kwenye Ndege, wanaotaka kuvua chini acha wavue, wale watani zetu (Simba) wanaotutania (Jangwani) wataaanza kuja kupiga selfie pale kwenye daraja na jengo la klabu yangu ya Yanga itaonekana." amesema