Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540883

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Makontena yenye makinikia yameshauzwa" Waziri Mkuu

Bungeni leo katika kipindi cha maswali Kwa Waziri Mkuu, Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusiana makontena yenye makinikia ambayo yameonekana yakisafirishwa kwenda nje ya Nchi kuwa makontena hayo yanasafirshwa kihalali.

“Watanzania kuyaona makontena yakipita na hofu ya awali nataka niwaondolee kuwa makontena yale yameshauzwa tayari na yule ni mnunuzi kwa hiyo waondoe mashaka juu ya usafirishaji wa makontena hayo yenye makinikia kwasababu Serikali iko makini sana inayo timu palepale kwenye mgodi kwa ajili ya uhakiki lakini pia ya mauzo na kuhakikisha fedha inalipwa na hakuna kontena linatoka nchini bila kuuzwa lakini pia tumeweka timu bandari hakuna kontena linaibiwa”———MAJALIWA

Join our Newsletter