Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 13Article 563017

Habari Kuu of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mali za Jambazi Maarufu Zapigwa Mnada

Mali za Al Capone Mali za Al Capone

Uuzaji wa mali za jambazi maarufu wa Marekani, Al Capone umekusanya jumla ya dola milioni 3 za Kimarekani (£ 2.2m) kwenye mnada uliofanyika mwishoni mwa wiki huko California.

Baadhi ya vitu 174 - pamoja na silaha za moto na picha za kibinafsi pamoja na vito na samani zimeonyeshwa. Hafla hiyo, inayoitwa Karne ya Umaarufu: Mali ya Al Capone, ilifanyika katika kilabu cha kibinafsi na ilivutia wazabuni karibu 1,000.

Bidhaa maarufu zaidi ilikuwa bunduki inayopendwa na Capone, ambayo iliuzwa kwa $ 860,000. Bunduki hii inaaminika ilkuwa bei ya juu zaidi ya silaha ya karne ya 20 iliyouzwa kwenye mnada, kulingana na Chicago Tribune.

Al Capone alikuwa mhalifu mkubwa Chicago aliyejulikana kama Adui Namba moja wa Umma kwa utawala wake mfupi kama kiongozi wa uhalifu miaka ya 1920. Mali ya Al Capone ilisalia katika milki ya familia yake kwa karibu miaka 75 baada ya kifo chake mnamo 1947.

Diane Capone - mmoja wa wajukuu watatu wa Al Capone walionusurika, ambao wanaishi California - alisema uamuzi wa kuuza vitu hivyo ulitokana na yeye na dada zake kuzeeka, kulingana na taarifa za shirika la habari la Reuters.