Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541279

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Maliasili na Utalii yatambia mafanikio 13

Maliasili na Utalii yatambia mafanikio 13 Maliasili na Utalii yatambia mafanikio 13

WIZARA ya Maliasili na Utalii imepata mafanikio makubwa 13 katika mwaka wa fedha 2020/2021, likiwemo la kupunguza ujangili na uvunaji haramu wa maliasili na hivyo kufikisha tembo 7,061 katika mwaka 2020 kutoka 6,087 kutoka mwaka 2014.

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma jana, Dk Damas Ndumbaro (pichani) alisema katika kipindi hiki wizara hiyo imeendelea kuimarisha ulinzi wa rasilimali za maliasili kwa kudhibiti ujangili, biashara haramu ya nyara, uvunaji haramu wa mazao ya misitu na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa shughuli za kilimo, ufugaji na makazi.

“Mathalan, matokeo ya sensa ya mwaka 2020 yameonesha kuongezeka

kwa idadi ya tembo katika Mfumo Ikolojia Serengeti kutoka 6,087 mwaka 2014 hadi 7,061 mwaka 2020,” alisema.

Dk Ndumbaro alisema, mafanikio ya kupungua kwa ujangili, uvunaji haramu wa mazao ya misitu na kuongezeka kwa wanyamapori yamechangiwa na kuendeshwa kwa siku doria 746,413 zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 5,609, kuvunjwa kwa mitandao 95 ya ujangili na kuzua matukio 302 ya ujangili kabla hayajatendeka.

Katika kutekeleza mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Mimea Vamizi (2019 - 2029), wizara kwa kushirikiana na wadau imeendelea kufanya utafiti juu ya mtawanyiko, madhara na kubaini mbinu za kukabiliana na mimea vamizi ndani ya hifadhi na maeneo yanayopakana na hifadhi.

Wizara pia imefanikiwa kuondoa mimea vamizi kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 2,269 katika

hifadhi za taifa za Arusha, Kitulo, Serengeti, Katavi, Milima ya Mahale, Ziwa Manyara, Mikumi, Milima ya Udzungwa, Ibanda

- Kyerwa, Rumanyika

- Karagwe, Tarangire, Gombe, Kitulo, Kisiwa cha Saanane na Kilimanjaro kwa lengo la kuboresha maeneo ya malisho.

Aidha, miti ya asili 2,700 imeoteshwa katika hifadhi za taifa Kilimanjaro na Kitulo katika maeneo ambayo mimea vamizi imeng’olewa.

Katika jitihada za kuhifadhi rasilimali za misitu, wizara imepandisha hadhi msitu wa Essmingori uliopo wilaya ya Monduli wenye hekta 6,070 kuwa hifadhi ya msitu ya mazingira asilia na hivyo kuongeza hifadhi za misitu ya mazingira asilia kutoka 19 hadi 20.

Aidha, wizara imepandisha hadhi maeneo 30 mapya ya misitu yenye ukubwa wa hekta 139,869 kuwa hifadhi katika wilaya za Chunya, Iringa,

Same, Korogwe, Lushoto, Handeni, Muheza, Mwanga, Buhigwe, Mkuranga, Chemba, Newala, Ileje, Dodoma, Ilala, Bukoba, Mbeya Vijijini, Butiama, Misenyi, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa, Madaba na Monduli.

Aidha, hifadhi za nyuki sita zenye ukubwa wa hekta 19,134 katika wilaya za Ileje, Handeni, na Chemba zimetangazwa na hivyo kuongeza idadi ya hifadhi za nyuki kutoka moja hadi saba.

Katika hatua hiyo ya kuboresha iundombinu ya huduma za utalii, barabara zenye urefu wa kilometa 73.4 zimejengwa na kilometa 8,599.8 zimekarabatiwa ndani ya maeneo ya hifadhi za taifa, eneo la hifadhi ya Ngorongoro, hifadhi za misitu ya mazingira asilia, mashamba ya miti, mapori ya akiba pamoja na vituo vya malikale.

Aidha, kambi za kitalii na loji zenye vitanda 670 zimejengwa katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa lengo

a kuboresha huduma za malazi na kuhamasisha utalii wa ndani. Wizara imefanikiwa kujenga malazi ya kitalii ya gharama nafuu yenye vitanda 105 katika hifadhi za taifa Saadani (71), Tarangire (12), Mkomazi (12) na Kitulo (10) kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.

Aidha alisema Tanzania imeendelea kupokea watalii licha ya uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa covid-19. Kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa sekta ya utalii nchini, katika mwaka 2020, wizara ilitarajiwa kupokea watalii 1,867,000. Makisio hayo yalikuwa ni kabla ya kutokea kwa janga la covid-19.

Baada ya mlipuko wa covid-19, wizara ilifanya tathmini ya athari za ugonjwa huo katika sekta ya utalii na kuweka makisio mapya ya watalii 437,000 yaliyozingatia hali halisi ya uwepo wa ugonjwa.

Join our Newsletter