Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 08Article 569245

Habari Kuu of Monday, 8 November 2021

Chanzo: globalpublishers

Mama Mzazi wa Hamza azikwa, Ndugu wafichua kilichomuua

Mama Mzazi wa Hamza azikwa, Ndugu wafichua kilichomuua play videoMama Mzazi wa Hamza azikwa, Ndugu wafichua kilichomuua

Mama mzazi wa kijana Hamza Mohammed aliyewashambulia na kuwaua askari wanne kwa risasi kisha na yeye kuuawa kwa kupigwa risasi nje ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Sofia Hassan amezikwa katika Makaburi ya Kisutu.

Bi Sofia alifariki dunia Novemba 7, 2021 katika Hospitali ya Muhimbili alikokimbizwa baada ya kuugua ghafla na kuzikwa siku moja baadaye, Novemba 8, 2021 majira ya saa saba mchana ambapo waandishi wetu Richard Bukos na Issa Mnally, wamefanikiwa kuzungumza kwa ufupi na mmoja wa wanafamilia hiyo.

Bi Sofia amezikwa kando ya kaburi la mwanaye, Hamza, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi Agosti 25, 2021 na kuzikwa Agosti 29, 2021 katika makaburi hayo ya Kisutu.