Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 15Article 557560

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 15 September 2021

Chanzo: millardAyo

Mama ashikiliwa kwa kumchoma mwanae moto

Mama ashikiliwa kwa kumchoma mwanae moto Mama ashikiliwa kwa kumchoma mwanae moto

Polisi Mkoani Manyara wanamshikilia Mwanamke mmoja baada ya kufanya kitendo cha kikatili kwa Mtoto wake wa kumzaa kwa kumchoma kwa moto chanzo kikiwa ni Mtoto huyo kuomba pesa kwa wapita njia.

RPC Mwakyoma wa Manyara amesema "Ilikua Babati Mjini Mtaa wa Mlala Juu Mtoto aitwae Neema Vicent wa miaka mitatu na miezi kumi na moja alichomwa moto na Mama yake sehemu mbalimbali mdomoni, shingoni na usoni, Mama yake aitwae Janeth Vicent alikasirishwa na kitendo cha Mtoto kuomba pesa kwa Wapita njia karibu na kwao"

"Wasamaria wema waliripoti kitendo hicho Polisi na Mama yake akakamatwa, Mtoto alifikishwa Hospitalini na kulazwa, Mama anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi, nitoe wito tusikimbilie kuadhibu Watoto, tukimbilie sana kuelimisha Watoto na kuwajengea Watoto tabia