Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585877

Editorial News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mambo Yanayoweza Kukusababishia Laana Kwenye Maisha yako

Mambo Yanayoweza Kukusababishia Laana Kwenye Maisha yako Mambo Yanayoweza Kukusababishia Laana Kwenye Maisha yako

1. Kumdhulumu Mtu: Jasho la mtu huzaa mikosi. Machozi na manung'uniko anayoyatoa Mtu aliyeumizwa kwa kudhulumiwa, hugeuka laana na kujikuta kila unachofanya hufanikiwi
-
2. Kuua au kutoa kafara: Damu ya Mtu ni laana, Damu ya Mtu ni mkosi, Damu ya Mtu ni nuksi. Ukisikia kuwa kuna vitu havina midomo lakini vinaongea, basi ni Damu ya Mtu. Kuna Watu wakifanya mauaji wanakosa nguvu za kukimbia na wengine hata kuwa kama aliyepoteza Akili
-
3. Kumkana au kumtukana Mzazi: Vitabu vya Mungu vinaeleza, "Waheshimu Baba na Mama upate kheri na miaka mingi Duniani". Kuna Watu wameshindwa kufanikiwa Maisha yao yote kutokana na laana ya Wazazi.