Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 13Article 557197

Habari Kuu of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maombi ya Jaji Mkuu Tanzania kuhusu gharama kubwa za "Internet"

Prof.Ibrahimu Juma, Jaji Mkuu Tanzania Prof.Ibrahimu Juma, Jaji Mkuu Tanzania

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof.Ibrahimu Juma, ametoa ombi kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, kupunguza gharama za intaneti ili kuwezesha Mahakama kufika katika Karne ya 21 inyo sukumwa na Mapinduzi ya nne ya Viwanda.

Ametoa ombi hilo wakati wa Shughuli za uapishwaji wa viongozi wateule wa serikali leo Septemba 13 ,2021 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

"Ninapenda nimuombe Waziri wa Tehama ambaye sisi Mahakama tunamtegemea sana kutusaidia kuingia katika karne ya 21, karne ambayo Rais uliwahi kusema inasukumwa na mapinduzi ya nne ya viwanda"- Jaji Mkuu

Aidha amefafanua kwa kueleza kuwa, Mahakama inategema Mkongo wa taifa utaendelea kuunganishwa na Mahakama hivyo wanaomba gharama za Intanenti zishuke ili waweze kufika katika malengo hayo.

"Mahakama inategea mkongo wa taifa utaendelea kuunganishwa na mahakama zetu gharama za 'internet' zitashuka kwasababu hiyo ndiyo barabara iliyobaki ya kufika katika hayo mapinduzi manne ya viwanda," amesema Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma