Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557410

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maombi ya Rais Samia kwa taasisi za dini, asasi za kiraia kuhusu Sensa

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, amewaomba viongozi wa dini, Asasi za kiraia, Mashirika yaliyo na yasiyo ya kiserikali pamoja na vyombo vya habari kuhakikisha wanawasisitiza wananchi juu ya umuhimu wa zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika kitaifa mwaka 2022.

Ametoa wito huo leo septemba 14, 2021, wakati wa ufunguzi wa zoezi la uhamasishaji wa Sensa linalofanyika kitaifa katika jiji la Dodoma.

Rais Samia amezitaka taasisi hizo kuisaidia serikali katika kutoa hamasa kwa wananchi kwani zoezi hilo ndio nguzo ya serikali katika kufikia mipango na mikakati iliyojiwekea.

"Niwaombe sana viongozi wa dini, kila mnapotoa mahubiri, msisahau kusemea suala la sensa, Niwaombe wadau wetu wa maendeleo wakiwemo Asasi za kiraia, na mashirika ya kimataifa, nanyi kushirikiana kwa pamoja kuhamasiha sensa, nipende kuviomba vyombo vya habari kuhamasisha sensa" Rais Samia

Amehitimisha kwa kuwaomba wasanii nchini pia, kuisaidia seriklai kuhamasisha wananchi kuhusu sensa.