Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 02Article 555007

Habari Kuu of Thursday, 2 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mapambano dhidi ya Ugaidi nchini yajadiliwa na Baraza la usalama Marekani

Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mkurugenzi  wa Usalama wa Taifa Marekani, Dana L. Banks Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Marekani, Dana L. Banks

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Msaidizi Maalum wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi katika Baraza la Usalama la Taifa Dana L. Banks.

Mazungumzo hayo yamelenga juu ya kuwawezesha wanawake kuhusu biashara ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mikakati ya kupambana na ugaidi.

Hatua hii inatazamiwa katika kufanikisha malengo hayo makuu yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita, katika kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kiuchumi kwa jinsia zote.